Bila shaka Alexis Sanchez anaonyesha kiwango cha juu sana kwa sasa na kuvutia watu wengi kumuangalia. Sasa ripoti kutoka Hispania ni kwamba manguli wa La Liga Real Madrid wanaendelea sera yao ya kutaka kusajili mastaa na Sanchez ana level hiyo kwa sasa kuanzia jina hadi uwezo wa uwanjani.
Real inasemekana inataka kutoa ofa ya £37 million kwa Arsenal pamoja na winger Denis Cheryshev kwa ajili ya kumpata Sanchez ambae anaisaidia sana Arsenal kwa sasa.Taarifa hizi hazijatoka official kutoka wa club ya Real Madrid lakini wapekuzi wa mambo ndio wamezidaka
Hizi ni tetesi ambapo mara nyingi kila habari kubwa huanzia kwa style hii. Lakini mashabiki wa Arsenal watazidi kuchukia kama mchezaji huyu akihama na uwezekano huo ni mdogo sana kwasababu Arsenal nayo inahitaji huduma yake.
Comments
Post a Comment