KOCHA wa Real Madrid, Rafa Benitez amekiri kuwa alizungumza na beki wake, Sergio Ramos kuhusiana na mpango wake wa kuondoka na kujiunga na Manchester United na akafanikiwa kumshawishi kubaki.
Beki huyo wa Santiago Bernabeu alitarajiwa kukamilisha uhamisho kwenda Man United, baada ya klabu hiyo ya Old Trafford kutenga pauni 28.6 kwa ajili ya nyota huyo wa Hispania.
Lakini baadae nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, aliamua kubaki La Liga.
Akizungumza na mtandao wa Onda Cero, Benitez alisema. "Nilipambana zaidi ya mwingine kwa ajili ya Ramos kubaki. Hakuna tatizo kati yetu.
Yeye ndie Nahodha wetu, mchezaji mwenye kiwango cha juu na ataendelea kuonyesha hilo."
Comments
Post a Comment