Nguvu ya wachezaji masupastaa Real Madrid huenda ikamtafuna kocha Rafa Benitez, hiyo ni baada ya nahodha Sergio Ramos kujibu mapigo ya shutuma za kocha huyo.
Benitez alishmtumu hadharani Ramos baada ya mchezo dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid na kusema nahodha huyo alipoteza mpira kizembe kipindi cha kwanza ambapo katika juhudi zake za kuukomboa mpira alioupoteza, akacheza rafu iliyosababisha penalti.
"Kilichonishangaza ni kosa la Ramos alipoporwa mpira kwa kufanya masihara kwenye eneo hatarishi," alisema kocha huyo katika mazungumzo yake na vyombo vya habari.
Ramos akajibu mapigo siku mbili baadae akiwa na timu ya taifa ya Hispania kwa kusema: "Tungeweza kuzungumza kuhusu makosa yangu au tungeweza pia kuzungumzia makosa yetu ya kubadilisha wachezaji (substitutions) katika mchezo. Wote tunajifunga kutokana na makosa, wachezaji na makocha."
Beki huyo alikuwa analenga 'sub' iliyofanywa na Benitez ya kumtoa mfungaji wa bao la Real Madrid Karim Benzima ambayo alidai ilichangia kuigharimu timu.
Kauli hiyo ya Ramos Ilikuwa ni kama angalizo tosha kwa Benitez - ukinilipua hadharani na mimi ntakulipua hadharani.
Sergio Ramos akwazana na kocha wake
Benitez alimshutumu Ramos hadharani kwa kusababisha goli la kusawazisha la Atletico Madrid
Ramos nae akajibu mapigo kwa Benitez
Comments
Post a Comment