Georginio Wijnaldum amefunga magoli manne kati ya sita yaliyoipa ushindi wa kwanza Newcastle kwenye Premier League dhidi ya Norwich.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya 6-2, Georginio Wijnaldum alifunga katika dakika ya 14, 26, 65, 85 huku magoli mengine yakifungwa na Ayoze Perez dakika ya 33 na Aleksandar Mitrovic kunako dakika ya 64 wakati yale ya Norwich yaliwekwa kimiani na Dieumerci Mbokani dakika ya 20 na Nathan Redmond dakika ya 35.
Ushindi huo wa Newcastle umekuwa ni ahueni kwa kocha
Steve McClaren ambaye kibarua chake kipo hatarini kutokana na mwenendo mbaya wa timu yake.
NEWCASTLE UNITED (4-4-2): Elliot 6; Janmaat 6, Mbemba 6, Coloccini 6, Dummet 6 (Haidara 64mins 6); Sissoko 7.5, Colback 7, Tiote 6.5 (Anita 45mins 6.5), Wijnaldum 8;Perez 7, Mitrovic 7 (Cisse 86mins 6).
NORWICH CITY (4-2-3-1): Ruddy 5.5; Whittaker 6, Martin 5.5, Bassong 5.5, Olsson 6 (Jerome 83mins 6); Dorrans 6 (O'Neill 83mins 6), Tettey 6 (Hoolahan 61mins 6); Redmond 7, Howson 6, Brady 6; Mbokani 7.
Georginio Wijnaldum amefunga mara nne dhidi ya Norwich wakati Newcastle ikishinda 6-2
Wijnaldum akishangilia moja ya magoli yake
Wijnaldum akiifungia Newcastle bao la kwanza kwenye dimba la St James' Park
Comments
Post a Comment