MWENYEKITI STAND UTD AKIRI LEIWIG HATAKI USHIRIKIANO



MWENYEKITI STAND UTD AKIRI LEIWIG HATAKI USHIRIKIANO
Kocha mkuu wa timu ya Stand United Patrick Leiwig

Kocha mkuu wa timu ya Stand United Patrick Leiwig

Mwenyekiti wa klabu ya wapiga debe wa Shinyanga Stand United maarufu kama 'chama la wana' Amani Vicent amekiri kuwa kocha mkuu wa timu hiyo mfaransa Patric Leiwing hataki kupewa ushari na viongozi wa timu hiyo pamoja na viongozi wenzake waliopo katika benchi la ufundi la timu hiyo.

Akizungumza na mtandao huu Amani amesema kocha huyo amekuwa akikaidi na kubeza ushauri unaotolewa na viongozi wa timu ambapo kauli hiyo imetokana na baada ya kocha huyo kujibizana vibaya na mwenyekiti wa timu alipo jaribu kumshauri kitu siku ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City shinyanga.

"Kiukweli huyu kocha sisi hatumuelewi maana ukitaka kumpa ushauri hataki anataka yeye afanye anavyo taka sasa hii inatupa shida kidogo maana imepelekea hadi kushindwa kuelewena na makocha wenzake lakini tutalifanyia kazi", amesema Amani.

Kocha mkuu wa Stand United Patrick Leiwig (kushto)              akiwa pamoja na mwenyekiti wa klabu ya Stand United Aman              Vicent

Kocha mkuu wa Stand United Patrick Leiwig (kushto) akiwa pamoja na mwenyekiti wa klabu ya Stand United Aman Vicent

Patrick Leiwing alipigwa faini ya shilingi millioni moja kufuatia kukiuka sheria za mchezo wakati Stand United ikicheza dhidi ya African Sport na pia kukataa kuongea na wanahabari.

Hivi sasa amemaliza kutumikia adhabu hiyo na yuko huru sasa, baada ya kutokuwa katika benchi la Stand kwa mechi mbili ambapo alikosa mechi za Simba na Mbeya City.



Comments