MWAMBUSI ATOA KAULI YAKE BAADA YA KUANZA KIBARUA JANGWANI



MWAMBUSI ATOA KAULI YAKE BAADA YA KUANZA KIBARUA JANGWANI
Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi (kushto)              akimuonesha kitu kocha mkuu wa timu hiyo Hans van der              Pluijm

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi (kushto) akimuonesha kitu kocha mkuu wa timu hiyo Hans van der Pluijm

Jana kocha Juma Mwambusi alianza rasmi kibarua chake kwenye kikosi cha Yanga wakati mabingwa hao watetezi wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya mabingwa wa Kagame Cup timu ya Azam FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii kwenye uwanja wa taifa.

Mwambusi amesema anashukuru kwa mapokezi mazuri ndani ya kikosi cha Yanga lakini akaomba apewe muda na ushirikiano na wanajangwani huku akiitanguliza Yanga mbele halafu wachezaji na mashabiki baadae.

"Namshukuru Mungu nimepokewa vizuri nadhani nitatoa ushirikiano wa kuweza kufanya kazi vizuri. Mwalimu Hans amefurahi kwasababu alikuwa anataka mtu mchapakazi na anasema siku nyingi amekuwa ananifatilia kwahiyo anafurahi kufanya kazi na mchapakazi kama yeye alivyokuwa anataraji", amesema Mwambusi ambaye kwa sasa ndiye kocha msaidizi wa Yanga.

"Mimi nataka nijifunze mengi kabla sijaingia sana mtamboni, mechi ya Jumamosi tunacheza na Azam ambayo tunaijua kwasababu tumeshacheza nao kwahiyo ni kupeana mawazo nini cha kufanya kwenye mechi hiyo ya Jumamosi".

"Nimekutana na wachezaji wangu niliowahi kuwafundisha Moro United, Mbeya City na wengine tukiwa tumekutana kwenye mechi lakini mambo yanakwenda vizuri na wao wamefurahi na kuonekana wanaungana na mwalimu ambaye walikuwa nae siku za awali".

"Kikubwa naomba nipate uhirikiano kutoka kwa wana-Yanga tushikamane, tupeane muda ili tuweze kufanya kitu kizuri, Yanga kwanza halafu wachezaji na mashabiki baadae".



Comments