NAHODHA wa timu ya soka ya Simba, Mussa Hassan 'Mgosi' amesema kikosi cha Wekundu hao kimesheheni wachezaji wa kiwango, hivyo ana imani na timu hiyo kufanya vema msimu huu.
Mgosi ameyasema hayo siku moja tu baada ya Simba kuvunja mwiko wa kutoondoka na ushindi jijini Mbeya, kwa kuwakandamiza Mbeya City bao 1-0 kwenye uwanja wa Sokoine.
"Huu ni mwaka wa Simba kung'ara na hata kutwaa tena ubingwa kwa msimu huu, hasa kutokana na matokeo ya michezo ambayo timu imecheza hadi sasa," alisema Mgosi.
Anasema, hadi sasa timu haijapata matokeo mabaya, licha kupoteza mchezo dhidi ya Yanga, wanachoangalia sasa ni kuona wanashinda katika mechi zijazo.
"Tumejipanga kuhakikisha azma ya kutwaa ubingwa kwa msimu huu maana Klabu ya Simba ni kubwa na inahitaji kucheza mechi za Kimataifa, hivyo njia pekee ni kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara," aliongeza Mgosi.
Comments
Post a Comment