Mesut Ozil amesisitiza kuwa Arsenal itaifunga Bayern Munich pale watakapokutana nao katika michuano ya Champions League.
Arsenal ipo kwenye hali mbaya katika kundi F na italazimika kuifunga Bayern Munich Oktoba 20 na Novemba 4 ili kufufua matumaini ya kusonga mbele.
Ozil anasema kama watacheza kwa ubora ule waliounyesha katika mchezo wa Premier League dhidi ya Manchester United basi Bayern lazima wakae.
Mesut Ozil (kushoto) anaamini Arsenal itaifunga Bayern Munich Champions League
Alexis Sanchez akishangilia bao dhidi ya Manchester United
Comments
Post a Comment