Mshambuliaji wa Manchester United Memphis Depay amesisitiza kuwa hasumbuliwi hata kidogo na wanaohoji kiwango chake Old Trafford.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Holland alijiunga na Manchester United msimu huu kwa pauni milioni 25 kutoka PSV Eindhoven huku akibebeshwa sifa kibao na kutegemewa kuwa mmoja wa nyota wakali barani Ulaya.
Akiwa PSV, Depay mwenye umri wa miaka 21, alifunga magoli 22 kwenye ligi kuu ya Holland, lakini hadi sasa ameshindwa kuonyesha makali yake kwenye Premier League.
Tayari baadhi ya wachambuzi na mashabiki wa soka wameanza kuhoji juu ya uwezo wa Depay lakini mwenyewe anasema changamoto hizo hazimnyimi usingizi.
Memphis Depay akikabiliana na mchezaji mwenzake wa Manchester United Daley Blind kwenye mazoezi ya Holland
Comments
Post a Comment