MEMPHIS DEPAY AKUBALI KWAMBA ANAPATA TABU KUZOEA SOKA LA ENGLAND


MEMPHIS DEPAY AKUBALI KWAMBA ANAPATA TABU KUZOEA SOKA LA ENGLAND

gettyimages-484410636-1-1024x704

Mategemeo kwa Memphis Depay wakati anakuja Manchester United yalikua makubwa sana kwa mashabiki wa Manchester united. Lakini Depay ameonekana kuwa ana struggle sana ku-adapt na ligi hiyo na kujikuta akichezea sub mara nyingi.

Akiwa kwenye press conference Depay alikubali hilo swala kwamba anapata tabu sana kuzoea ligi ya England. "Siku za mazoezi unakuwa unawaza kuwa vizuri tu kwa ajili ya mechi. Ni ngumu sana kuwa kwenye EPL, mechi mbili kila wiki na unatakiwa kuwa tayari. Kwasababu hiyo mwili wangu haujazoea hivyo ndio maana nazoea taratibu. Lakini siku zote nitasema nina furaha sana kuwa Manchester united. Najaribu kwenda mbele kila siku kwenye maisha yangu ya soka, nadhani hii ilikua ni step nzuri"



Comments