Hatimaye uvumilivu umemshinda kocha msaidizi wa Manchester United, legendari Ryan Giggs na kuamua kumpa onyo kijana huyo kutokana na mwenendo wake ndani ya Manchester United hivi sasa.
Manchester United walitoa pauni milioni 25 kwa kijana huyo (21) kutoka PSV Eindhoven lakini alitolewa nje muda wa mapumziko Manchester United ikiadhibiwa na Arsenal kwa magoli 3-0 wiki iliyopita.
Chanzo kimesema kuwa Depay baada ya mchezo wa Arsenal alionekana usiku akila bata huku akionesha kutojali kwa mambo yanayoendelea uwanjani.
Giggs ametoa onyo kwa kijana huyo kutuliza akili na kufikiria zaidi uwanjani kuliko nje ya uwanja. Giggs amesema hayo huku akimkumbuka kocha wake Sir Alex Ferguson aliyekua mkali sana kwa wachezaji aina ya Depay.
Aidha akiongea na gazeti moja la nchini Uholanzi, Depay anasema amebadilisha mazingira na kwamba anahitaji muda kuzoea ligi kwani ni ngumu na kila mechi imekua na uzito mkubwa huku akidai kwamba hakuna muda wa kupumzika hata mazoezi na kwamba mwili wake unahitaji muda wa kupumzika.
Comments
Post a Comment