MASHABIKI WA ARSENAL WANA KILA SABABU YA KUFURAHIA


MASHABIKI WA ARSENAL WANA KILA SABABU YA KUFURAHIA

ss
Kama wewe ni shabiki wa club fulani basi lazima utakua una-wish mchezaji wa club yako asipate majeraha akienda kwenye mechi ya timu ya taifa. Lakini kwa Arsenal wana sababu ya ziada ya kufurahia zaidi ya wachezaji wao wengi kumaliza salama.

Ukicheki magoli au assist nyingi za tiku mbalimbali zimefanikishwa na wachezaji wa Arsenal. Maana yake ni kwamba timu nzima ya Arsenal ipo kwenye form nzuri ambapo wachezaji wao wanazisaidia timu zao kupata ushindi. Uwezo huo wanaounyesha kwenye timu zao unategemewa kuendelea kwenye mechi za Arsenal.

Ukicheki kwenye takwimu za haraka ni kwamba Alexis amefunga magoli 3, Ozil ametoa assists 2, Cazorla amefunga mara mbili, Giroud amefunga mara 2, Ramsey katupia moja, Chamberlain moja, Walcott moja, Akpom moja, Gnabry moja, Campell moja.

Pia kitu cha kuchekesha zaidi wale walioikimbia Arsenal kama Fabregas kakosa penati, Van Persie kajifunga basi ni shida tupu.



Comments