Timu mbili zinazotesa kwa kuwa na wachezaji wa bei mbaya, Manchester United na Manchester City zimetoka sare ya bila magoli katika mchezo uliodorora wa Premier League.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Old Trafford ulishuhudia timu hizo zikitengeneza nafasi chache sana za kufunga.
Kwa sare hiyo, City inarejea kileleni mwa msimamo wa ligi ikiipiku Arsenal kwa wastani wa magoli.
Mshambuliaji wa Manchester United Jesse Lingard nusura aipe ushindi timu yake dakika za lala salama pale mpira wake wa kichwa ulipogonga mwamba
MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 6.5 (Darmian 5.5), Jones 6.5, Smalling 7, Rojo 6.5; Schweinsteiger 7(Fellaini 6.5), Schneiderlin 6; Mata 5 (Lingard 7), Herrera 6.5, Martial 7; Rooney 5.5.
MANCHESTER CITY (4-2-3-1): Hart 6.5; Sagna 6.5, Kompany 7, Otamendi 8, Kolarov 6; Fernando 6, Fernandinho 6.5; De Bruyne 6, Toure 6 (Demichelis 6), Sterling 5.5 (Navas 6); Bony 5(Iheanacho 6).
Comments
Post a Comment