Manchester City imeendelea kutakata kwenye michuano mbalimbali baada ya kuibugiza Crystal Palace 5-1 katika Capital One Cup huku supastaa wao mpya Kevin De Bruyne akiendelea kuwa tishio.
Kevin De Bruyne aliifungia City kunako dakika ya 44 ikiwa ni baada ya mashambuliaji wa Kinigeria Wilfried Bony
kuifungia timu hiyo bao la kwanza dakika ya 22.
Kelechi Iheanacho mwenye umri wa miaka 19, raia wa Nigeria aliyeigharimu City pauni 350,000, alifunga bao la tatu katika dakika ya 59 kabla ya Toure na Garcia hawajafunga dakika ya 76 na 90 huku bao pekee la Crystal Palace likifungwa na Delaney dakika ya 89.
Iheanacho ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo baada kutandaza soka safi na kupiga magoli kadhaa.
MANCHESTER CITY (4-4-2): Caballero 5; Zabaleta 7 (Sagna 56, 6), Mangala 6.5, Demichelis 7, Kolarov 6; Navas 6.5, Toure 6, Fernando 6, De Bruyne 7 (Roberts 75, 6); Iheanacho 8, Bony 5.5 (Garcia 84)
CRYSTAL PALACE (4-5-1): Hennessey 5; Kelly 5.5, Dann 5, Delaney 6, Mariappa 5 (Ward 85); Zaha 6.5, Jedinak 6, Mutch 5 (Chung-yong 75, 6), Ledley 5, Bolasie 6.5; Bamford 5 (Gayle 77, 6)
Kinda wa Manchester City Kelechi Iheanacho alikuwa nyota wa mchezo kwa kufunga mara moja na kupika mabao mawili katika ushindi wa Capital One dhidi ya Crystal Palace
Chipukizi Manu Garcia, 17, alitokea benchi na kuifungia City bao la tano ndani ya dimba la Etihad Stadium Jumatano usiku
Beki wa Crystal Damien Delaney akiruka hewani na kuifungia timu yake bao pekee
Nahodha wa Manchester City Yaya Toure akifunga bao la nne
Iheanacho akifunga goli la tatu kwa City
Staa wa Manchester City Kevin De Bruyne akifunga bao la pili
Wilfried Bony alikuwa wa kwanza kuifungia City bao la kuongoza akiunganisha kona ya Aleksandar Kolarov
Comments
Post a Comment