KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Manchester United, Loius Van Gaal amesema kuwa kuwapo kwa wachezaji majeruhi kunamuumiza kichwa.
Gaal alisema hayo jana wakati akizungumza na badhi ya vyombo vya habari na kudai kuwa amegundua kuna pengo katika kikosi chake.
Alisema tatizo hilo limechangia kupoteza baadhi ya michezo na wakati mwingine kuishia kuambulia sare.
"Wachezaji kuumia mara nyingi husababisha matatizo makubwa, lakini najaribu kupambana ili kuhakikisha namaliza tatizo hilo kwa kujaribu kuwapa mbinu za kukwepa kuumia uwanjani," alisema Van Gaal.
Comments
Post a Comment