Kibarua cha Jose Mourinho kinazidi kuning'inia pabaya baada ya Chelsea kufungwa 3-1 na Liverpool kwenye uwanja wao wa nyumbani - Stamford Bridge.
Bosi huyo wa Chelsea alijaribu kila mbinu kuwarejesha wachezaji wake kwenye kiwango chao lakini mwisho wa siku pointi tatu zikaondoka.
Chelsea ilikuwa ya kwanza kufunga katika dakika ya 4 kupitia kwa Ramires lakini wakati timu hiyo ikiamini kuwa inakwenda mapumziko ikiwa mbele, Coutinho akasawazisha dakika ya 45.
Coutinho akaendelea kuwa mwiba kwa Mourinho kunako dakika ya 74 pale alipofunga bao la pili kabla ya Benteke hajahitimisha ushindi saba kabla mchezo haujamalizika.
Huu unakuwa ushindi wa kwanza kwenye Premier League nna wa pili mfululizo katika michuano yote kwa kocha mpya wa Liverpool Jurgen Klopp.
Chelsea (4-2-3-1): Begovic 6; Zouma 5, Cahill 6, Terry 6, Azpilicueta 6 (Falcao 75, 6); Ramires 7, Mikel 6.5 (Fabregas 69, 6), Willian 7; Oscar 6.5, Hazard 5 (Kenedy 59, 6), Costa 6
Liverpool (4-3-3): Mignolet 6; Clyne 7, Skrtel 7, Sakho 7.5, Moreno 5.5; Can 6.5, Lucas 6.5, Milner 7 (Benteke 64, 7); Lallana 7.5 (Lovren 90), Coutinho 8.5, Firmino 7.5 (Ibe 75, 6.5)
Philippe Coutinho (kulia) akiifungia Liverpool
Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza Coutinho baada ya kuisawazishia Liverpool
Coutinho akifunga bao la pili
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao la pili ndani ya Stamford Bridge
Christian Benteke akihitimisha ushindi wa Liverpool
Chelsea wakishangilia bao lao
Comments
Post a Comment