KOCHA WA MALAWI AICHIMBA ‘MKWARA’ STARS MECHI YA MARUDIANO


KOCHA WA MALAWI AICHIMBA 'MKWARA' STARS MECHI YA MARUDIANO
Ernest Mtawila, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Malawi              'The Flames'

Ernest Mtawila, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Malawi 'The Flames'

Baada ya kupokea kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa Stars, kocha wa Malawi Ernest Mtawila amesema, mechi ilikuwa ngumu na Stars ilijipanga kuhakikisha inapata ushindi wa nyumbani lakini akasisitiza kuwa bado wanamatumaini ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano wakiwa kwenye uwanja wao wa nymbani.

"Mechi ilikuwa ngumu lakini nadhani Tanzania walijipanga vizuri kupata ushindi wa nyumbani, haikuwa rahisi kwa upande wetu hasa baada ya kuruhusu magoli mawili ndani ya kipindi cha kwanza lakini naamini tunaweza kubadili matokeo tukiwa Malawi", amesema Mtawila.

"Nimeridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wangu, tulichea mechi Jumatano na baadhi ya wachezaji wangu wanaocheza Afrika Kusini walikuwa na mechi Jumapili. Kwahiyo walikuwa na siku moja pekee ya kupumzika kabla ya kuingia kwenye mchezo huu, kuna baadhi ya wachezaji walikuwa wamechoka".

"Tulifungwa magoli ya haraka mwanzoni mwa kipindi cha kwanza lakini kwa mabadiliko tuliyofanya kipindi cha pili, yalitusaidia tukacheza vizuri".

"Jumapili tutakuwa kwenye uwanja wetu wa nymbani nadhani tutatumia faida ya kucheza kwenye uwanja wa nyumbani".  



Comments