KOCHA MALAWI AMUOTA ALLY MUSTAFA ‘BARTHEZ’


KOCHA MALAWI AMUOTA ALLY MUSTAFA 'BARTHEZ'

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Malawi, Ernest Mtawali amesema timu yake imekosa nafasi ya kuitoa Taifa stars, kutokana na umahiri wa kipa Ally Mustafa 'Barthez'.
Alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na vyombo vya habari nchini humo, kuhusu sababu ya wao kushindwa kuitoa Tanzania katika mechi za awali za mtoano kuelekea makundi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018.
"Tuseme ukweli, kipa wa Tanzania ndio ametunyima ushindi, alikuwa kizingiti tangu mchezo wa kwanza hadi mechi ya marudiano hapa Blantyre," alisema.
Alisema uwezo wa kipa huyo upo juu na kwamba anaamini akipata wakala mzuri anaweza kutafutiwa timu ya kucheza barani Ulaya.
Aliongeza kusema anaamini hata Algeria wasipokuwa makini mbele ya kipa huyo namba moja kwa sasa wa Yanga na taifa Stars, watahadhirika.


Comments