KLOPP HAONI KAMA MECHI YA LIVERPOOL VS CHELSEA NI KUBWA




KLOPP HAONI KAMA MECHI YA LIVERPOOL VS CHELSEA NI KUBWA

Klopp vs Mourinho

Kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp amesema kwa mtazamo wake inachezwa mechi kati ya timu zilipo katika nafasi ya 9 na 15 kwenye msimamo wa ligi, hivyo kama ni ukubwa labda kihistoria.

Chelsea walio katika nafasi ya 15 leo hii wanawakaribisha Liverpool walio katika nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi katika uwanja wa Stamford Bridge mechi yenye umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili kupata pointi tatu, lakini presha ikiwa kubwa kwa Jose Mourinho wa Chelsea anayetetea kibarua chake.

Lakini Klopp ambaye alikua katika hali kama hiyo aliyonayo Mourinho hivi sasa, wakati huo Klopp akiwa Dortmund msimu uliopita anasema kuwa anamuonea huruma Mourinho lakini akasema kuwa timu yake imejiandaa kushinda.

Kuhusu ukubwa wa mechi, Klopp anasema kuwa hajasoma magazeti kujua namna mechi hii ilivyoandikwa lakini akasema kama ni ukubwa basi ni katika historia na wala sio sasa.

Mechi kati ya Liverpool na Chelsea ni miongoni mwa fixture kubwa katika soka la Uingereza kwa kipindi cha muongo mmoja sasa. Lakini leo wanakutana timu zote zikiwa haziko katika ubora tuliozizoea.



Comments