JURGEN KLOPP SASA NI RASMI MALI YA LIVERPOOL ...mkataba wa miaka mitatu, mshahara wa pauni mil 4 kwa msimu
Jurgen Klopp ametua Merseyside Alhamisi mchana tayari kwa kukamilisha mkataba wake wa kuwa kocha mpya wa Liverpool.
Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, amekubali dili linatalotajwa kuwa ni la mkataba wa miaka mitatu utakaompatia mshahara wa pauni milioni 4 kwa msimu.
Klopp anatarajiwa kutambulishwa rasmi Liverpool siku ya Ijumaa saa 4 asubuhi.
Jurgen Klopp ametua Merseyside Alhamisi mchana tayari kwa kukamilisha dili lake la kuikochi Liverpool
Klopp (katikati) mara baada ya kuwasili John Lennon Airport huko Liverpool
Ndege iliyombeba Klopp ikitua Liverpool
Comments
Post a Comment