Sasa Jurgen Klopp anaanza kupata experience ya vyombo vya habari vya England ambapo picha moja tu inaweza kutengeneza story kubwa zaidi ya kawaida.
Klopp baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari alitumia muda wa usiku wa Ijumaa kwenda kwenye pub moja kupata glass moja, basi hapo akajaliwa na mashabiki wa kike wanne na kupiga nae picha.
Picha hiyo ikaanza kuleta maswali kuhusu jina lake la The Normal One, lakini ripoti za uhakika zinasema hao wakina dada hawakua na Klopp bali walimuona na kujitambulisha kama mashabiki wa Liverpool. Kilichofuata ni picha na kocha wao.
Comments
Post a Comment