Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp may anategemewa kuwa boss wa Liverpool ndani ya siku chache zijazo, lakini utambulisho wake rasmi Anfield hautakuwa ndiyo mara yake ya kwanza kukanyaga kwenye ardhi ya klabu hiyo.
Jurgen Klopp alitua Liverpool kwa mara ya kwanza August 10 ya kiangazi kilichopita wakati klabu yake ya zamani Borussia Dortmund ilipokwenda Anfield kucheza mchezo wa kirafiki na Liverpool kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya.
Ni kama vile mashabiki wa Liverpool walikuwa wanabashiri kitu flan kwa namna walivyomlaki na kukumbatia Klopp kwa bashasha huku wengine wakimpiga picha kupitia kamera na simu zao.
Je urafiki huo wa mashabiki wa Liverpool kwa Jurgen Klopp utaendelea baada ya kocha huyo kukalia kiti cha moto Anfield? Ni jambo la kusubiri.
Jurgen Klopp alipolakiwa na mashabiki wa Liverpool mwaka 2014 wakati alipokwenda na Borussia Dortmund katika mchezo wa kirafiki
Kocha Borussia Dortmund enzi hizo, akisani picha za mashabiki wa Liverpool
Kocha aliyetimuliwa Liverpool Rodgers akikumbatiana na Klopp anayetarajiwa kuwa mrithi wake, hiyo ilikuwa ni mwaka 2014 ambapo Liverpool iliichakaza Dortmund 4-0 katika mchezo wa kirafiki ulipigwa Anfield
Comments
Post a Comment