Jurgen Klopp ameanza na kauli tata kwenye mkutano wake wa kwanza wa waandishi wa habari akiwa kama kocha mpya wa Liverpool, pale aliposema yeye ni "The Normal One" akimaanisha mtu wa kawaida.
Hiyo inakuwa ni kama kijembe kwa Jose Mournho wa Chelsea ambaye wakati anajiunga na na klabu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2004 alijiita "The Special One" (mtu wa kipekee).
Klopp, ambaye amesisitiza kuwa atakuwa na kauli ya mwanzo na ya mwisho katika usajili wa wachezaji, alisema neno hilo pale alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo na yeye ni Special One kama Mourinho.
"Sitaki kujiita kitu chochote," alisema Klopp. "Mimi ni mtu wa kawaida, hata mama yangu anautazama mkutano huu. Kama unataka kuniita kitu chochote, niite mtu wa kawaida."
Jurgen Klopp akitambulishwa rasmi Liverpool Ijumaa asubuhi
Klopp akiwa kazungukwa na jezi za Liverpool
Klopp katika mkutano wa kwanza wa waandishi wa habari akiwa kama kocha mpya wa Liverpool
Comments
Post a Comment