JINA LA MBWANA SAMATTA NDANI YA ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA


JINA LA MBWANA SAMATTA NDANI YA ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA
Mbwana Samata

Mbwana Samata

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ali Samatta leo ametajwa katika listi ya wanasoka wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika. 

Samatta ambaye anakipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Congo, ametajwa kwenye listi hiyo ambayo imetolewa na shirikisho la soka la Afrika – CAF

Samatta ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuelezea furaha yake juu ya uteuzi huo na kuomba aombewe dua ili tuzo ije Tanzania.

Mchezaji huyo leo alikuwa katika kikosi cha Tanzania kilichocheza na Malawi katika mechi ya pili ya kuwania nafasi ya kucheza kwenye kombe la dunia 2018 na kufanikiwa kuiwezesha Taifa Stars kusonga mbele kwa jumla ya magoli 2-1.

IMG_9250.PNG



Comments