Beki wa kimataifa wa Belgium na klabu ya Tottenham Jan Vertonghen jana alipigwa picha akiletwa mazoezini na mama yake, tukio ambalo limeleta kumbukumbu nyingi za utotoni mwake.
Katika wakati ambao wachezaji wa soka huwa wanajaribu kufunikana kwa kwenda mazoezini wakiwa na magari ya kifahari, kitendo cha Vertonghen kupelekwa na mama yake mzazi na gari la kawaida kabisa ni cha aina yake.
Gari hilo linunuliwa na wazazi wa Vertoghen miaka 9 iliyopita na kwa bahati mbaya mzazi wa kiume wa Vertoghen alifariki dunia wiki kadhaa baadae na tangu wakati huo mama mzazi wa mwanasoka huyo aliahaidi kutokuliuza hilo gari japo lilifikia hatua ya kuharibika kabisa – lakini mama huyo aligharamika kulitengeneza kwa kununua vifaa vingi vipya na sasa limeimarika.
Vertoghen hamiliki gari la aina yoyote nchini Belgium na mama yake amemkataza kununua gari akiwa nchini mwao kwa sababu halitokuwa likitumika kwa muda mwingi kwa sababu anapendelea kutumia Toyota Corolla ambayo waliinunua na mumewe – hivyo anapendelea kuitumia gari hiyo kama kumbukumbu ya mumewe kipenzi.
Comments
Post a Comment