Lewandowski na Aubameyang wameshafunga magoli 13 hadi sasa na vichwa vya habari vinatawaliwa na majina yao hasa kuhusu Bundesliga. Sasa ukizungumzia kufumania nyavu bado wana safari ndefu sana kuvunja rekodi ya mkongwe Gerd Müller ambae anashikiria rekodi ya kufunga magoli 40 kwenye msimu mmoja.
Hii ilikua kwenye msimu wa 1971-72 ambapo alikua mshambuliaji wa Bayern Munich alifumania nyavu mara 40 rekodi hiyo hadi leo bado haijavunjwa. Hadi sasa Lewandowski na Aubameyang wameshacheza mechi 10 na kufunga mara 13 na zimebaki mechi zaidi ya 30 hadi msimu uishe. Kama wakiendelea na kasi hii hii kuna uwezekanao wakavunja rekodi ya mkongwe huyu.
Comments
Post a Comment