HIVI NI VITU BINAFSI VYA ROBERT LEWANDOWSKI AMBAVYO ULIKUA HUVIJUI


HIVI NI VITU BINAFSI VYA ROBERT LEWANDOWSKI AMBAVYO ULIKUA HUVIJUI

968786_toptease_article_desktop

Sasa hivi kila mtu anamjua Lewandowski kwa uwezo wake wake wa kutupia magoli nyavuni kwa idadi kubwa. Hivi hapa ni vitu ambavyo amevisema Lewandowski kuhusu yeye na watu wengi walikua hawavijui.

Lakini kabla ya kujua kuhusu huyu jamaa, kumbuka kwamba ataingia uwanjani kwa mara nyingine tena na club yake ya Bayern kucheza dhidi ya Werder Bremen siku ya Jumamosi saa 10:30. Kila mechi ya Bundesliga Startimes wamekupa nafasi ya kuangalia hizo mechi Live kwa gharama utakayoimudu mtanzania wa kawaida.

Damu ya michezo
Lewandowski ana damu ya michezo kwasababu baba yake Krzystof alikua bingwa wa mchezo wa Judo na mama yake Iwona alikua ni mcheza Volleyball wa kulipwa. Dada yake pia aliwai kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Poland kwenye mchezo wa Volleyball. Kwa hiyo michezo ipo kwenye damu ya familia

Msiba mkubwa
Lewandowski anasema kwamba kwenye maisha yake alimpoteza baba yake ambae alikua mtu muhimu sana kwa wakati huo akiwa na umri wa miaka 16. "Baba yangu alifariki ghafla nikiwa na miaka 16, ilibidi mimi ndio niwe baba wa nyumba kwa kipindi kile. Kila nikiwa nafanya mazoezi msukumo mkubwa naupata nikimkubuka yeye"

Mtoso kwa mara ya kwanza
Feanciszek Smuda kocha wa zamani wa Lech Poznan alienda mara mbili kwenda kumuangalia mchezaji mdogo ambae ndio Lewandowski akiwa anacheza soka. Kwenye moja ya safari alimwambia mtu wake wa scouting aliyempeleka kumuangalia Lewandowski kwamba itabidi amlipe pesa zake za mafuta kwa kumpotezea muda kwenda kumuangalia Lewandowski. Kosa kubwa alilifanya kocha yule ambae leo hii anamuona Lewandowski akicheka na nyavu na kukumbuka kwamba hakuona kipaji cha mchezaji huyo hapo zamani.

Kuanza utawala ndani ya Borussia
Lewandowski alifunga magoli 8 kwenye msimu wa kwanza wa Bundesliga akiwa na Borussia. Sasa msimu uliofuatia alifunga magoli 30 na kufanikiwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha BVB. Lewandowski alifanikiwa kumuondoa  Lucas Barrios kwenye kikosi cha kwanza cha Borussia na kuchukua nafasi yake.

Mpenzi wake
Lewandowski michezo ipo hadi nyumbani. Mpenzi wake Anna Stachurska amewai kushinda medali ya Shaba kwenye mashindano ya Karate. Pia mwanamke huyu ni mtaalamu wa mambo ya virutubisho vya chakula (Professional Nutritionist). Wawili hawa wanafananishwa sana na Beckham na Victoria lakini tofauti yao hawa wanapenda maisha ya private badala ya kuanika kwenye magazeti.



Comments