Hivi ndivyo vilabu 3 vya ulaya Pele aligoma kwenda kuvichezea


Hivi ndivyo vilabu 3 vya ulaya Pele aligoma kwenda kuvichezea

Mshindi wa mara tatu wa kombe la dunia, Pele, anafahamika na wengi kama mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Kwa pamoja na Diego Maradona, Pele anatajwa kuwa mwanasoka bora zaidi huku akimpiku Maradona kwa mataji matatu ya dunia. 

 Pele ana rekodi ya kufunga magoli yapatayo 1,000 katika maisha yake ya soka, lakini kuna kitu kimoja ambacho hakuwahi kufanikiwa – kucheza soka barani ulaya, mahala ambapo soka linatajwa kuwa katika kiwango cha juu. 

  Pele alibaki kucheza nchini Brazil na America katika kipindi chote cha maisha yake, akigoma kwenda kucheza Ulaya katika vilabu vikubwa ili kuongeza mshahara wake maradufu. 

Akiongea na kituo cha habari cha Brazil, O Rei, alifunguka kwamba alipiga chini ofa nzuri kutoka kwa vilabu kadhaa barani ulaya ili kuthibitisha mapenzi yake kwa klabu yake ya Santos. 

  Fikiria kikosi ambacho kingekuwa na  Best, Charlton na Pele katika safu ya ushambuliaji – hii ni ndoto ambayo ingetimia kama Pele angekubali ofa ya kujiunga na Manchester United pindi ilipomtaka.

  'Ni kweli mwanasoka inabidi utengeneze maisha baada ya soka, lakini kwangu mimi hasa wakati nikicheza soka ilikuwa tofauti. Nilipata ofa nzuri sana za kujiunga na vilabu vya Manchester United, Real Madrid, AC milan lakini Santoa ilikuwa kila kitu kwangu, timu ilikuwa ikicheza vizuri nami pia nilikuwa nacheza vizuri hivyo sikutaka kuondoka.' – PELE 



Comments