HIVI NDIVYO JINSI EPL INAVYOONGOZA KWA MAPATO ULIMWENGUNI


HIVI NDIVYO JINSI EPL INAVYOONGOZA KWA MAPATO ULIMWENGUNI

EPL MapatoLigi kuu nchini England (EPL) ndio ligi inayoongoza kwa maingizo (mapato) makubwa zaidi ulimwenguni hivi sasa kutokana na kuwa na mikataba minono na makampuni makubwa zaidi ulimwenguni.

Hivi sasa ligi hiyo iko mbioni kusaini mkataba wa kuuza haki za maonesho ya TV kwa ligi yao yenye thamani ya pauni billion tatu kwa miaka mitatu 2016-19 kwa wastani wa pauni billion kwa mwaka.

Mkataba wa sasa uliosainiwa mwaka 2013-16 ni wa pauni billion 2.23 kwa misimu hiyo mitatu sawa na pauni milioni 743 kwa mwaka.

Takwimu zinaonesha kwamba ligi kuu England inapata mapato mengi zaidi ya TV kutoka nje ya England kuliko ligi kuu yeyote ile duniani (La liga, Serie A, Bundesliga, League 1 na Ureno) ambapo mapato ya TV ya ndani na nje ya ligi hizi nyingine hayafikii mapato ya nje pekee ya TV ya ligi kuu England.

Nchini Marekani kwa mfano, shirika la utangazaji la NBC pekee lilinunua haki ya kurusha matangazo ya ligi hiyo maarufu zaidi duniani kwa pauni milioni 250 kwa kipindi cha kuanzia 2013-16. Shirikisho hilo linatarajia ku-renew mkataba utakaonzia 2016-22 wenye thamani ya pauni 1bn.

Hong Kong pia ni sehemu maarufu sana hivi sasa kwa soko la TV la ligi kuu ya England ambapo kutokana na tours za vilabu vya England nchini China imefanya ligi hiyo kuwa na mashabiki wengi zaidi nchini humu kitu kinachopelekea mapato makubwa zaidi kwa ligi hii maarufu duniani.

Hong Kong imekua ni sehemu muhimu zaidi nje ya England kwa mauzo mazuri ya haki za TV za EPL. Siri hapa ni namna tozo zinavyokatwa kwa wateja wanaotaka kutizama mechi za ligi kuu England.

Umaarufu wa EPL barani Asia kwa ujumla ni neema na utajiri wa ligi hii pendwa duniani, huku vilabu vyake vikinufaika na mapato na kuwa na nguvu kiuchumi.

Nchi kama za Thailand, Malaysia, Singapore, India na Indonesia ni maeneo yenye fan-base kubwa sana ya vilabu vinavyoshiriki ligi kuu nchini England.



Comments