HENRY AITABILIA MEMA ARSENAL MSIMU HUU



HENRY AITABILIA MEMA ARSENAL MSIMU HUU
Nguli wa Arsenal Thiery Henry anaamini kuwa timu yake                ya zamani (Arsenal) itanyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu England                msimu huu
Nguli wa Arsenal Thiery Henry anaamini kuwa timu yake ya zamani (Arsenal) itanyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu
Nyota wa zamani wa Arsenal Thiery Henry anaimani kubwa kwamba huu ni msimu ambao Arsenal wanapaswa kutwaa 'ndoo' ya EPL na kumaliza ukame wa miaka takriban 11 ya ubingwa wa EPL.
Miamba hao wa London Kaskazini kwa sasa wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa EPL nyuma ya Manchester City lakini wakitofautiana kwa idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga wakishinda michezo yao yote minne ya mwisho ya ligi.
Vijana hao wa Arsene Wenger wameshinda michezo yao minne kwa ushindi wa kishindo dhidi ya Leicester City, Manchester United na Watford, wakati huo huo wakiwafunga mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya huku wakionesha soka la ushindani wa hali ya juu katika siku za hivi karibuni hasa katika mechi zenye ushindani mkubwa.
Akiongea na TalkSPORT Jumanne wiki hii, Henry aliongea kwa kujiamini kuhusu timu yake hiyo ya zamani kunyakua ubingwa, akisema: 'Nasema kwa dhati kabisa huu ni mwaka wao. Wanapata matokeo dhidi ya timu kubwa sasa na matokeo hayo yanawapa nguvu kubwa ya kujiamini. Hilo ndio jambo kubwa'.
Viwango bora vya Olivier Giroud na Theo Walcott ni mchango mkubwa sana kwa matokeo mazuri ya Arsenal katika siku za karibuni huku washambulizi hao wakionekana kuchuana vikali hali inayoongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji miongoni mwao.
'Theo Walcott kucheza kama mshambuliaji wa kati kunamsukuma Giroud aongeze juhudi, na vivyo hivyo kwa Giroud.'
Henry pia amewapongeza Mesut Ozil, Santi Cazorla Hector Bellerin na Petr Cech kwa viwango vyao bora ambavyo ndio mchango mkubwa kwa matokeo mazuri ya klabu hiyo.


Comments