HENDERSON NDIYE ALIYEPEWA JUKUMU LA KUWAAMBIA WACHEZAJI WA LIVERPOOL JUU YA KUTIMULIWA KWA BRENDAN RODGERS
Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson ndiye aliyebebeshwa jukumu la kuwaeleza wachezaji wenzake juu ya kutimuliwa kwa kocha Brendan Rodgers.
Kiungo huyo wa England alipewa jukumu hilo baada ya sare ya 1-1 kwa Everton Jumapili iliyopita.
Inaaminika kuwa baada ya wachezaji wa Liverpool kuduwazwa na habari hizo, wakafurahi pale walipobaini ujio wa kocha Jurgen Klopp ambaye wanaamini anaweza akaipa makali klabu yao.
Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson (kushoto) ndiye aliyewasilisha kwa wachezaji wenzake habari za kutimuliwa kwa kocha Brendan Rodgers
Comments
Post a Comment