Guus Hiddink amekataa kukanusha uwezekano wa kuifundisha Chelsea iwapo Jose Mourinho ataondoka Stamford Bridge.
Kocha huyo Mdachi aliwahi kuifundisha kwa muda Chelsea mwaka 2009 na kushinda taji la FA.
Kwasasa Guus Hiddink hana kazi baada ya kujiuzulu kuifundisha timu ya taifa ya Holland na alipoulizwa iwapo atapenda kufundisha Premier League, Hiddink alisema hiyo ni nafasi adimu ambayo hawezi kuitupa.
Mourinho yuko kwenye shinikizo kubwa baada ya kuwa na mwanzo mbaya msimu huu ikiwa ni pamoja na kutupwa nje kwenye michuano ya Capital One Cup.
Guus Hiddink yupo tayari kuikochi Chelsea kama Jose Mourinho atatimuliwa
Jose Mourinho yuko kwenye shinikizo kubwa Chelsea
Hiddink alipokuwa akiifundisha kwa muda Chelsea
Hiddink alipoipa Chelsea taji la FA Cup
Msimamo wa Ligi Kuu ya England ukionyesha timu sita za mwisho Chelsea ikiwemo
Comments
Post a Comment