Inaelezwa kuwa kocha Loius Van Gaal amepata hofu juu ya winga wake mholanzi Memphis Depay na kuogopa asije akaishia kama Di Maria na kuwa flop Old Trafford.
Van Gaal anasema ana imani na kijana huyo lakini akasema tatizo la wachezaji wenye umri mdogo ni kutokuwa na consistency uwanjani.
Van Gaal anasema Ryan Giggs ni winga bora zaidi wa kizazi chake katika upande wa kushoto na kusema kuwa tayari amekwishaanza kumsaidia Depay acheze katika misingi itakayomfanya awe mchezaji mzuri.
"Ryan anamsaidia Memphis, awe ni mchezaji bora na muhimu hapa. Anahitaji kubadilika na kuwa consistent"
Kocha Van Gaal alikataa kuchangia katika ugomvi uliotokea baina ya Depay na Robin Van Persie wakiwa katika timu ya taifa ya Uholanzi wiki iliyopita.
Aidha Memphis Depay alipigwa benchi na kocha huyo katika mechi ya ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Everton Goodson Park hapo jana huku akimuingiza pia kipindi cha pili kinda Jese Ringard kichukua nafasi ya Juan Mata.
United sasa itasafiri jumatano hii kwenda Moscow Urusi kumenyana na CSKA Moscow katika muendelezo wa michuano ya klabu bingwa ulaya.
Comments
Post a Comment