Kocha legendari wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Wayne Rooney atarudi katika fomu yake na kuanza kufunga magoli.
Fergie amesema hayo ikiwa ni wakati ambao uwezo wa Rooney ukiwa umepungua hivi sasa huku akiwa na goli moja tu kati ya michezo 13 ya ligi kuu England.
Mzee huyo anasema siri ya washambuliaji ni 'confidence' na kwamba ndio kitu kinachomsumbua Wayne Rooney hivi sasa. Anasema washambuliaji wakiwa wanafunga hujiamini kwamba wataendelea kufunga siku zote, lakini pia wasipokua wanafunga, hufikiri hawawezi funga tena.
Sir Alex anasema hayo yaliwakuta mastraika wote, Nistelrooy, Cole, Cantona huku akikumbuka hata yeye enzi zake uwanjani kwamba kujiamini ndio siri ya kurudi kwenye fomu.
Akiwatoa hofu mashabiki wa Manchester United, Sir Alex anasema anaamini Rooney atakuja upya na kuanza kufunga tena kama anavyomjua.
Aidha akiongea kuhusu Wayne kuwa nahodha wa United, Fergie anasema hakuna mtu mwingine mwenye sifa za cheo hicho kikosini kuzidi Wazza.
Comments
Post a Comment