Mara baada ya ushindi wa timu ya taifa ya Hispania wa magoli 4-0 dhidi ya Luxembourg jana usiku katika kuwania nafasi ya kushiriki fainali za kucheza michuano ya mataifa ya Ulaya EURO 2016, Cesc Fabregas aliandika rekodi ya kipekee katika timu hiyo.
Fabregas akicheza mchezo wake wa 99 katika timu hiyo, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye assists nyingi (pasi nyingi za mwisho/magoli) kuliko mchezaji mwingine yeyote wa nchi hiyo.
Fabregas ameweka rekodi hiyo baada ya kutoa assists 28 akiwa na kikosi cha Hispania akiivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na nyota wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Xavi Hernandez.
Saint Carzola na Paco Alcacer walifunga mara mbili kila mmoja na kuipa ushindi timu yao ambayo sasa imefuzu rasmi kucheza fainali hizo zitakazo pigwa nchini Ufaransa mwakani.
Habari mbaya katika mchezo huo ni majeruhi ya kiungo wa Manchester City David Silva ambaye alitolewa nje katika dakika ya 9 tu ya mchezo baada ya kuumia kifundo cha mguu 'ankle' na nafasi yake kuchukuliwa na Juan Mata.
Taarifa za Silva ni pigo kwa City ambao tayari watamkosa Sergio Aguero katika mechi dhidi ya Manchester United katika mchezo wa ligi wiki mbili zijazo.
Comments
Post a Comment