ENGLAND MOTO WA KUOTEA MBALI, YAENDA EURO 2016 KWA STAILI YA AINA YAKE ...Lithuania achukua tatu bila
England imefuzu kwenda Euro 2016 kwa staili ya aina yake baada ya kushinda mechi zake zote 10 katika hatua ya makundi.
Hiyo ni baada ya Lithuania kukubali kichapo cha 3-0 mbele ya England iliyojikusanyia jumla ya pointi 30 na magoli 31 huku ikiwa imeruhusu nyavu zake kutikisika mara tatu tu.
Goli la kwanza la England lilifungwa na kiungo wa Everton Ross Barkley kunako dakika ya 29 kabla ya kipa Giedrius Arlauskis hajajifunga dakika ya 35 katika juhudi zake za kuokoa.
Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain akaihakikishia ushindi England baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 62.
LITHUANIA (4-2-3-1): Arlauskis 6.5; Freidgeimas 5, Mikuckis 5.5, Kilmavicius 6.5, Andriskevicius 5.5 (Vaitkunas 82mins); Panka 5, Zulpa 6.5; Novikovas 6 (Petravicius 62, 6.5), Slivka, 5, Cernych 6.5; Spalvis 7 (Matulevicius 85)
ENGLAND (4-3-3): Butland 6.5; Walker 5.5, Jones 6, Jagielka 6.5, Gibbs 6.5; Barkley 8 (Townsend 73, 6.5), Shelvey 5.5, Lallana 7 (Alli 67, 5.5); Oxlade-Chamberlain 7, Kane 7 (Ings 59, 6), Vardy 6
Harry Kane (wa pili kulia) akipongezwa na Phil Jones baada ya juhudi zake kuchangia goli la pili la England
Ross Barkley (kushto) akipongezwa na Adam Lallana (right) baada ya kuifungia England bao la kwanza
Msimamo wa kundi E
Comments
Post a Comment