Mwanasoka bora England msimu uliopita Eden Hazard amesugua benchi wakati Chelsea ikirejesha upya makali yake kwenye Premier League kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Aston Villa.
Hazard alikaa benchi hadi dakika ya 83 wakati huo Chelsea ikiwa imeshavuna mabao yake mawili na ndipo nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alipoingia kuchukua nafasi ya Pedro.
Diego Costa akaifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 34 kabla ya beki wa Aston Villa Alan Hutton hajajifunga dakika ya 54.
CHELSEA 4-2-3-1: Begovic 6; Azpilicueta 6.5, Zouma 6, Terry 6, Baba 5; Ramires 7, Fabregas 6; Willian 6.5 (Remy 90), Loftus-Cheek 5 (Matic HT, 6), Pedro 6.5 (Hazard 83); Costa 7.5.
ASTON VILLA 4-2-3-1: Guzan 5; Hutton 5, Richards 5, Lescott 5, Richardson 5 (Amavi 64, 5); Westwood 5, Gueye 5; Gill 6, Grealish 6, Ayew 5 (Traore 69, 5); Gestede 5.
Diego Costa akipunga baada ya shuti lake kusababisha goli la pili dhidi ya Aston Villa
Cesc Fabregas (kushoto) akikimbia na mpira kushangilia baada ya Alan Hutton kujifunga
Comments
Post a Comment