Supastaa wa Chelsea Eden Hazard amekiri kuwa anapita katika kipindi kigumu baada ya kushindwa kucheka na nyavu katika michezo 10 ya mwanzo msimu huu.
Hazard, ambaye aliifungia Ubelgiji katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Androrra, ameshindwa kurejea kwenye 'fomu' iliyomwezesha kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Premier League msimu uliopita.
Kiungo huyo mchezeshaji mwenye umri wa miaka 24, amesema hajui ni kwanini anacheza chini ya kiwango lakini akasema bado yupo kwenye ari ya hali ya juu ili kurejesha makali yake.
Eden Hazard yupo kwenye kipindi cha mpito
Hazard akiifungia Ubelgiji
Comments
Post a Comment