Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Sunderland na Queens Park Rangers za England, Djibril Cisse ametangaza kustaafu soka na kuangusha kilio kupitia matangazo yaliyokuwa yakirushwa 'live' na televisheni ya Ufarsansa.
Cisse ambaye amechezea timu ya taifa ya Ufaransa mara 41 pamoja na vilabu 12 ndani ya miaka 15, ameamua kustaafu baada kucheza kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kufunga hata goli moja la ligi.
Mshambuliaji huyo mtukutu akashindwa kuyazuia machozi yake wakati kocha wake wa zamani Guy Roux alipokuwa akizungumza machache ya kumsifia.
Cisse mshindi wa Champions League akiwa na Liverpool, aliyetwaa kiatu cha dhahabu mara mbili Ufaransa na Ugiriki, alitumikia miaka mitano kusakata kabumbu ndani ya England ambapo alizichezea Liverpool aliyoifungia magoli 24, Sunderland na Queens Park Rangers.
Licha ya kutikisa nyavu mara 250 kwa nchi yake na vilabu, lakini hakufunga hata goli moja la ligi kuu msimu uliopita ingawa aliifungia klabu yake mabao matatu kwenye michuano mingine.
Cisse alianza soka lake kwenye klabu Auxerre wakati kocha Roux alipompa nafasi kwenye kikosi cha kwanza akitokea kwenye academy ya timu hiyo.
Djibril Cisse akilia wakati alipokuwa anatangaza kustaafu soka
Cisse akipambana kuyazuia machozi
Cisse alitumia misimu miwili iliyopita akiwa na Bastia lakini hakuweza kufunga hata goli moja la ligi tangu April 2014
Cisse atakumbukwa vizuri katika muda wake alioitumikia Liverpool na kufunga magoli 24 ndani ya misimu miwili
Hapa Cisse akiwa na medali ya Champions League baada ya Liverpool kuishinda AC MIlan mwaka 2005
Comments
Post a Comment