Mjerumani Jurgen Klopp anakabiliwa na mtihani wa kuirudisha Liverpool katika chati yake ya kuwa tishio ulaya baada ya kusaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho kwa misimu mitatu.
Kocha huyo amembadili Brendan Rodgers aliyekua akikinoa kikosi hicho bila ya mafanikio kwa misimu miwili iliyopita na hatimaye kufukuzwa juma lililopita.
Klopp ambaye alijiuzulu kuifundisha Borrusia Dortmund msimu uliopita anatarajiwa kutambulishwa leo kwa vyombo vya habari mara baada ya kusaini mkataba jana Alhamisi.
Katika hali isiyo ya kawaida, klabu ya Borrusia Dortmund kupitia ukurasa wake wa Twitter imemtakia kila la kheri kocha huyo katika maisha yake mapya na Liverpool.
Dortmund walipost picha ya mjerumani huyo huku wakimtakia kila lenye heri. Liverpool nao waliwajibu wenzao wa Dortmund kwa furaha waliyokua nayo kwa kupokea ujumbe huo.
Kocha huyo sasa ataanza mtihani wake wa kwanza dhidi ya Tottenham Hotspur weekend ijayo katika mchezo wa ligi kuu England ugenini White Hart Lane.
Comments
Post a Comment