DAVID BECKHAM amemwambia mshambuliaji wa England na Manchester United Wayne Rooney ahamie nafasi ya kiungo ili kulinda kiwango chake.
Rooney amekuwa hatabiriki msimu huu ambako amekuwa akipita katika nyakati mchanganyiko - nzuri na mbaya.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hadi sasa hivi ametupia wavuni goli moja tu katika Premier League.
Beckham kiungo wa zamani wa Manchester United amesema bado ana imani na Rooney lakini akamtaka asogee nafasi ya kiungo ili kupata uwanja mpana zaidi wa kuonyesha kipaji chake.
David Beckham amesema Rooney ana uwezo wa kumiliki na kusambaza mipira na hivyo kwa sasa eneo la kiungo ndiyo sehemu muafaka kwake.
Comments
Post a Comment