CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI YA RAUL ...sasa ndiye mchezaji mwenye magoli mengi Real Madrid kuliko yeyote yule
Hatimaye Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya Raul na kuwa mfungaji mwenye magoli mengi zaidi katika historia ya Real Madrid.
Ronaldo amevunja rekodi hiyo baada ya kufunga bao moja kwenye ushindi wa Real Madrid wa 3-0 kwenye La Liga dhidi ya Levante.
Ronaldo ameifungia Real Madrid jumla ya magoli 324 katika mechi 310 akimpiku Raul aliyefunga mara 323 katika mechi 741 alizoichezea Real Madrid.
Vipi kama Ronaldo angeichezea Real Madrid mechi 741 kama Raul, si ingekuwa balaa? Kungekuwa na mafuriko ya magoli.
Ronaldo akiifungia Real Madrid bao la 324
Ronaldo akipongezwa na wenzake baada ya kuvunja rekodi ya magoli Real Madrid
Comments
Post a Comment