CHUJI AWAAMBIA HIVI MASHABIKI WA MWADUI


CHUJI AWAAMBIA HIVI MASHABIKI WA MWADUI
Kiungo wa Mwadui FC Athumani Idd 'Chuji' (katikati)              amewaambia mashabiki wa Mwadui FC wasubiri mambo mazuri              kutoka kwa timu hiyo licha ya kuanza ligi kwa kusuasua

Kiungo wa Mwadui FC Athumani Idd 'Chuji' (katikati) amewaambia mashabiki wa Mwadui FC wasubiri mambo mazuri kutoka kwa timu hiyo licha ya kuanza ligi kwa kusuasua

Na Philipo Chimi, Shinyanga

Nahodha wa timu ya mwadui FC kutoka ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ,Athumani Idd 'Chuji' amewataka mashabiki wa timu hiyo wasubiri kuona mambo makubwa yakifanywa na wachezaji wa timu ya Mwadui katika msimu huu wa ligi kuu bara.

Akizungumza na mtandao huu, kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Yanga, amesema timu yao imejipanga kufanya vizuri hasa katika mechi zake za nyumbani licha ya kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Azam FC.

"Sisi kama wachezaji wa Mwadui tumejipanga kufanya mambo makubwa katika ligi msimu huu kwasababu hapa kunawachezaji wazuri na wenye uzoefu wa ligi, japo najua lig ni ngumu lakini mashabiki watulie tutawaonyesha kazi Octoba 17 dhidi ya JKT Ruvu", amesema Chuji.

Chuji akijifua uwanjani Mwadui Complex, Shinyanga

Chuji akijifua kwnye uwanjani wa Mwadui Complex, Shinyanga

Nae mshambuliaji machachali wa timu hiyo Paul Nonga amesema anafurahia maisha yake akiwa katika timu hiyo ya wachimba alimasi Mwadui FCU licha ya kuwa na ukame wa magoli ukilinganisha na hali ilivyokuwa Mbeya City msim uliopita.

"Nafurahi sana kuwa nyumbani unajua mimi nimezaliwa Shinyanga kwa hiyo nafurahi sana kucheza home, naomba mashabiki wangu watulie nitafanya mambo ligi bado ipo mwanzo sana", alisema mshambulianji huyo.

Paul Nonga kwa sasa anagoli moja tu ambalo alifunga dhidi ya African Sport mchezo uliochezwa katika uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga.



Comments