CARRAGHER: ARSENAL, MAN UNITED, KUTOLEWA CAPITAL ONE CUP NI BARAKA KWAO


CARRAGHER: ARSENAL, MAN UNITED, KUTOLEWA CAPITAL ONE CUP NI BARAKA KWAO
Jamie Carragher, mchezaji wa zamani wa Liverpool
Jamie Carragher, mchezaji wa zamani wa Liverpool
Jamie Carragher anaamini kwamba kutolewa kwa Arsenal na Manchester United katika kombe la Capital One ni baraka kubwa kwao.
Beki huyo wa zamani wa Liverpool anahisi kwamba kuondolewa kwa miamba hiyo katika moja ya michuano wanayoiwania ni fursa nzuri sana kwao kuwapiku wapinzani wao wakubwa Man City kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu England.
Arsenal almaarufu kama 'The Gunners' walitupwa nje ya michuano hiyo Jumanne wiki hii na timu ya Sheffield Wednesday wakati huohuo Man United wakipoteza mchezo wao dhidi ya Middlesbrough usiku wa jana.
 Ushindi wa Man City wa mabao 5-1 dhidi ya Crystal Palace una maana ya kwamba matajiri hao wa jiji la Manchester wanakutana na Hull katika hatua ya robo fainali.Wayne Rooney akitembea kwa masikitiko baada ya kukosa penati katika mchezo wa jana dhidi ya Middlesbrough.
Wachezaji wa Middlesbrough Grant Leadbitter, Ben Gibson na wenzake wakishangilia ushindi
Olivier Giroud na Mathieu Flamini wakionekana wenye huzuni baada ya kutupwa nje na Sheffield Wednesday.


Comments