ALIYEKUWA Kocha mkuu wa timu ya soka ya Liverpool, Brendan Rodgers amesema kuwa hana kinyongo chochote na uongozi wa timu hiyo kumfuta kazi.
Rodgers aliyasema hayo wakati akizungumza na gazeti moja la nchini humo kuwa yeye amekubali maamuzi hayo.
Alisema kuwa, hawezi kupinga kwavile wale ni waajiri wake na hawezi kupinga jambo lolote ambalo wanalitaka.
"Siwezi kusema kitu chochote kwavile wameamua kuniondoa, basi niangalie mambo mengine ya kufanya katika maisha yangu," alisema Kocha huyo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Kocha huyo kufutwa kazi na uongozi wa Klabu hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Jurgen Klopp.
Comments
Post a Comment