INGAWA waswahili husema, maneno sio mkuki, lakini msanii wa kike anayeheshimika ndani ya Nollywood, Bimbo Akintola amekiri kuchomwa na kuumizwa na maneno yanayosemwa kuwa, anajikondesha ili apendeze.
Bimbo amesema, kupungua kwa mwili wake kunatokana na kujichimbia kwa saa tatu kila siku, kwenye mazoezi Eko Gym pamoja na kutingwa na utengenezaji wa filamu yake mpya.
"Maneno ya watu kuwa najikondesha yananichoma na kuniumiza sana, kwa kweli mwili wangu umepungua kutokana na mazoezi mazito pamoja na ratiba ngumu ya kutengeneza filamu yangu mpya," alisema Bimbo.

Comments
Post a Comment