Barcelona imeitungua Rayo Vallecano 5-2 katika mchezo mkali wa La Liga huku mshambuliaji Neymar akifunga mabao manne.
Kwa magoli hayo, Neymar sasa anakuwa mfungaji mwenye magoli mengi zaidi La Liga msimu huu akiwa kishadumbukiza wavuni mabao 8.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil alifunga mara mbili kwa penalti ambazo zote alizisababisha yeye katika kipindi cha kwanza wakati magoli mengine aliyafunga kwa njia ya kawaida kipindi cha pili kutokana na kazi nzuri ya Luis Suarez.
Rayo Vallecano ndiyo waliokuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Javi Guerra dakika ya 15 kabla ya Barcelona haijacharuka na kufunga dakika ya 22, 32, 69 na 70 kupitia kwa Neymar huku Suarez akifunga bao la tano dakika ya 77 kabla Rayo Vallecano hawajapunguza maumivu kwa bao lao la pili lililofungwa na Jozabed.
Neymar akifunga bao la pili kwa penalti
Neymar (kushoto) akishangilia moja ya magoli yake sambamba na Suarez
Comments
Post a Comment