Aston Villa imemtimua kocha wake Tim Sherwood sambamba na wasaidizi wake Mark Robson na Ray Wilkins.
Watatu hao wamepigwa chini na mtendaji mkuu wa klabu Tom Fox ikiwa ni baada ya mwenendo mbaya kwenye Premier League.
Aston Villa ilalazwa 2-1 na Swansea Jumamosi na kuganda kwenye eneo hatarishi la kushuka daraja baada ya vipigo sita msimu huu.
Tim Sherwood ametimuliwa Aston Villa
Kibarua cha Sherwood kilikuwa hatarini tangu mwezi uliopita baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya
Kocha msaidizi Ray Wilkins naye pia ametimuliwa kazi
Comments
Post a Comment