ASTON Villa ni kama vile wanataka kutikisa mibuyu ya soka duniani, kwani sasa akili yao ni kutaka kumnasa nyota wa Real Madrid ya Hispania, Jese Rodriguez.
Habari zinasema kuwa, nyota huyo ambaye anawindwa pia na klabu kubwa, anaweza kuhamia katika klabu hiyo kwa njia rahisi zaidi.
Gazeti moja la michezo nchini Hispania la AS, limesema kuwa Aston Villa imewekeza nguvu nyingi katika usajiri mwezi Januari.
Habari hizo zinadai kuwa, Tim Sherwood amekuwa akiumiza kichwa kutazama namna gani kikosi chake kitakuwa imara zaidi na kwamba mapendekezo ya kusajili wachezaji wapya yapo mezani.
Hata hivyo mchezaji huyo ambaye pia amekuwa akiwindwa na Arsenal, Chelsea, Inter Milan pamoja na Napoli, amekaririwa akisema kuwa anataka kumalizia maisha yake La Liga na kwamba msimu ujao anataka kuhamia katika Ligi nyingine.
Wakala wa Jese Rodriguez amesema kuwa, anataka kumuongoza kuondoka Hispania na kusonga mbele, lakini akafichua kuwa ni Aston Villa ndio wenye nafasi kubwa ya kumsajili nyota huyo.
Jese Rodriguez ameshuka mara tatu tu katika kikosi cha Real Madrid na kwamba anajua maisha yake katika kikosi hicho hayako sawasawa.
"Anahitajika kucheza kwa kiwango kikubwa zaidi, lakini lazima acheze mechi nyingi zaidi, na kama mechi hizo hazipati hapa, lazima tutafute nafasi nyingine zaidi," amesema wakala huyo, Giones Carvajal.
Comments
Post a Comment