WAKATI Ligi Kuu ya England ikiendelea, klabu kubwa nazo zinafanya kila njia kusaka majina muhimu ambayo yatawasaidia katika msimu ujao.
Taarifa zinasema kuwa, Arsenal inaelekea kufanikiwa kuipiga kumbo Chelsea katika kumsajili nyota mahhiri, Donyell Malen katika dirisha lijalo la msimu wa kiangazi, ikiwa ni mapendekezo ya nguli wa zamani wa klabu hiyo, Dennis Bergkamp.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, nyota huyo amekuwa akizivutia sana klabu hizo mbili kubwa na kwamba mazungumzo na klabu yake ya Ajax yamekuwa yakionekana kuibeba Arsenal.
Malen ambaye amekuwa akicheza katika kikosi cha pili cha Ajax anatajwa kama mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuzivutia klabu hizo.
"Kuna kila uwezekano akahamia Arsenal, hii ina maana kuwa klabu nyingine zinaweza kumkosa," amesema Meneja wake.
Kocha wa Arsenal Wenger amezungumza na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Bergkamp, ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa Ajax, kuhusiana na umahiri wa mchezaji huyo.
Mazungumzo hayo yamedaiwa kuwa yamefikia mahali pazuri na kwamba Arsenal sasa inatakiwa kuilipa Ajax pauni mil 1.8 kwasababu bado kinda huyo mahiri wa kupachika mabao, ana mkataba wa miaka mitatu.
The Gunners wamekuwa na matumaini ya kumnyaka na kumwendeleza Malen na kuwa nyota mkubwa badae, ingawaje kwa miaka ya hivi karibuni klabu hiyo imekuwa ikidaiwa kuharibu mfumo wake wa kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi.
Comments
Post a Comment